DRC

UWANJA WA NDEGE WA GOMA KIVU KASKAZINI MASHARIKI MWA CONGO KARIBU NA MPAKA WA DRC NA RWANDA WASHAMBULIWA KWA BOMU MBILI

FEBRUARI 17, 2024
Border
news image

Uwanja wa ndege wa Goma Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo karibu na Mpaka wa DRC na Rwanda washambuliwa kwa bomu mbili .

Ni tangu saa nane za usiku mlio wa bomu kubwa ulisikika mara pili Katika Mji wa Goma Kivu kaskazini .kwa bahati mbaya bomu hizo zilikuwa zikilenga ndege za Kivu za DRC kwa Jina maalum SOkoi ambazo zimekuwa ziki pambana kwa muda mrefu ma waasi wa M23 kwenye milima ya Masisi.hadi sasa vyombo vya uslama vya DRC vyaendelea na uchunguzi kuhusu shambulizi hilo mbaya ambalo laweka kutishia usafari wa ndege .

Uwanja wa ndege wa Goma unapokea ndege nyingi za Kimataifa kutoka mataifa mbali mbali n ahata ikiwa njia moja muhimu kuunganisha Kinshasa na Mikoa ya mashariki mwa Congo .shambulizi la Bomu kwa uwanja wa Goma inazusha wasiwasi kubwa kwa wakaazi wanao ishi karibu na uwanja huo Pamoja na wamiliki wa ndege ambazo zipo katika uwanja huo.

Mbali na shughuli za kawaida uwanja wa ndege wa Goma wasaidia Vikosi vya Umoja wa Matifa yaani MONUSCO kuunganisha mikoa kadhaa ya mashariki mwa Congo ambako hakuna barabara.pamoja na hayo Uwanja wa ndege wa Goma ndio umebaki njia moja ya kungia Goma baada ya barabara zote kufungwa na kudhibitiwa na waasi wa M23 ambao serikali ya Kinshasa yasema wana saidiwa na Taifa La Rwanda.

Wakaazi wa kata Moja la Vuhene kaskazini mwa Uwanja huo tulio zungumuza nao wasema ,usiku walisikia sauti kubwa ikipita kwenye paa zao na dakika chache kukawa mlipuko ambao kila mmoja hakufahamu wapi umetokea.dakika chache ikagundulika bomu imeanguka katika uwanja wa ndege .

Baadhi ya marubani wa ndege na watu wa usalama wa anga walio hifadhi jina wanasema shambulizi kama hilo ni mbaya na laweza kusababisha kambuni za ndege kusitisha safari zake Mji Ngoma iwapo hakuna hatua kubwa kuhusu usalama wa ndege .

Mji wa Goma kwa sasa unazingirwa kwa sehemu kubwa na waasi wa M23 .

Lakini bado Ndege nyingine zaenelea na safari zake .

Serikali ikienelea na uchunguzi kuhusu Bomu hizo mbili zilizo anguka katika Mji wa Goma.

Shughu za ushafirishaji kwa ndege zaenelea kama kawaida hadi sasa bila wasiwasi yoyote.

AM/MTV DRC ONLINE