DRC - WIZARA YA VIWANDA

Uturuki Na Congo DRC Yaanza Ushirikiano Katika Ujenzi Wa Viwanda DRC

SEPTEMBA 14, 2023
Border
news image

Katika Mkutano ulio fanyika Mjini Kinshasa kati ya Waziri wa viwanda Julien Paluku Kahongya na ujumbe kutoka serikali yay a Uturiki wamezungumzia miradi muhimu na maalum ya Kiuchumi inayotekelezwa na Serikali ya Kongo inavutia wawekezaji zaidi wa Uturuki.

Alhamisi hii, Waziri wa Viwanda, Julien Paluku Kahongya alizungumza na kikundi cha wawekezaji wa Uturuki kutoka kampuni ya ALBAYRAK inayofanya kazi katika nyanja kadhaa ikiwa ni pamoja na sekta ya kilimo cha chakula, sekta ya mbao na usafi wa mazingira inayoongozwa na Canan Sahbaz.

Miundombinu inayotolewa na kanda maalum za kiuchumi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na uendeshaji wa kanda chache ikiwa ni pamoja na majaribio ya Maluku ambayo ilizindua uzalishaji wake wa viwanda ilikuwa katikati ya mkutano huu.

AM/MTVNEWS