Baada ya Rais wa Congo Felix Tshiskedi na Paul Kagame wa Rwanda kukutana Doha Quatar kukutana, hii juma tatu elfu mbili ishirini na tano, hatua ya usitishwaji mapigano yachukuliwa. Viongozi hao wamekubali kurudi katika mazungumuzo ya Angalo na mchakato wa mazungumuzo ya Nairobi kwenye kwani haina maana yoyote mzozo kuendelea kati ya mataifa mawili Jirani.
Mazungumuzo hayo kati ya viongozi wa wili imejiri baada ya waasi wa M23 kushushia mkutano ulio itishwa na msuluhishi wa mzozo wa mashariki mwa Congo DRC ambako kwa Zaidi ya miaka mitatu jeshi la Congo limekuwa likitwana na waasi wa M23 ambao Umoja wa Matifa na ripoti za umoja wa nchii za ulayani za shutumi taifa la Rwanda kuunga mkono uasi huo.
Mapigano ya muda mrefu mashariki mwa Congo DRC imesababisha, Vifo, Ubakaji na kupelekea watu wengi kupoteza maisha na wengine kubaki yatima wakilazimishwa kukimbia vijiji vyao na kuwa wakimbizi wa ndani yaani katika taifa lao.
Mkutano wa Paul Kagame wa Rwanda na Felix Tshisekedi wa Congo DRC unategemewa na wakaazi wengi hasa wale wanao kuwa eneo la mapigano inayo sababisha uporaji wa mali, ubakaji na mauaji ya watu.
Waasi wa AFC/M23 wakiwa wamechukuwa sehemu kubwa mashariki mwa Congo ikiwemo Mji wa Goma mji mkuu wa Kivu Kaskazini, Bukavu mji mkuu wa Kivu Kusini Pamoja na miji na vijiji kadhaa. Wakiendelea wilayani Walikale Kivu Kaskazini.