Akizungumuza na wanahabari katika Mji wa Goma Janez Lenarčič kamisheni wa EU ahusikae na misaada Pamoja na maswala ya amani asema Umoja wa Ulayani walaani vikali hatua ya Rwanda kuendelea kuleta vikosi vyake kwenye ardhi ya Congo nah ii haikubaliki.
Janez Lenarčič alisema Rwanda yapashwa kuwaondoa wanajeshi wake na watu wote wa serikali ya Rwanda ambao kwa sasa wako eneo linalo dhibitiwa na M23 pamoja na kuacha uungwaji mkono M23 .hata hivyo mataifa mengine ya kikanda nayo lazima kusitisha uungwaji mkono kwa makundi ya waasi mashariki mwa Congo.
Baada ya kukutana na gavana wa Kijeshi Kivu Kaskazini ujumbe wa Ulaya umeomba hata hivyo kundi la FDLR kuwa tishio kwa usalama wa taifa lazima serikali ya Congo kusitisha uhusiano wake na kundi hilo ambalo Rwanda imekuwa ikisema ndio sababu yake ya kuja DRC.
Wakiwa ziarani Mjini Goma wajumbe hao wametembelea kambi ya wakimbizi ya Bushagala ambako kwapatikana maelefu ya wakaazi kutoka ,Nyiragongo,Rutshuru baada ya kuhama makaazi yao kutokana na vita kati ya M23 na jeshi la Serikali FARDC.
Wakaazi walio kimbia makaazi yao wakiomba amani na usalama ili warudi nyumbani kwao kuliko kubaki kambini ambako Maisha ni maguku ,wengi wakibakwa na wengine wakiwa wagonjwa na kushuhudia ukosefu wa chakula.