DRC

Umoja wa mataifa yaani MONUSCO nchini DRC waomba kushirikishwa katika operesheni za kijeshi dhidi ya wapiganaji wa ADF wilayani Beni

news image

Viviane van de Perre, naibu mkuu wa MONUSCO anayehusika na operesheni na ulinzi, alizungumza na mamlaka ya kiraia na kijeshi ya DRC na viongozi wa jumuiya kuhusu suala la usalama mashariki mwa DRC. Nakuomba ushirikiano wa MONUSCO na Fardc katika kuwafuatilia ADF kwenye misitu ambako wamekimbilia kwa sasa.

"Lengo lilikuwa kujadili ushirikiano na FADC, na hasa kuimarisha juhudi zetu za pamoja dhidi ya nguvu hasi," hasa ADF. MONUSCO imedhamiria vipi kutekeleza jukumu lake la kulinda raia na kusaidia vikosi vya ulinzi na usalama vya Kongo.

Katika mapambano dhidi ya makundi yenye silaha", alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jumanne, Novemba 12 katika mji wa Beni.

Haya yanasemwa huku muungano wa Frdc na UPDF ukifanya kazi kubwa katika maeneo ya mapigano na kugomboa vijiji vyote ambavyo vilikuwa vimeikaliwa na ADF na kwa sasa wakaazi wakiwa wameanza rudi mashambani kwao.

Wakaazi wengi wasema hawatakubali MONUSCO kungia tena katika msako wa ADF kwani muda mrefu wamekaa Beni wakiwa katika uangalizi wa mauaji ya raia na hawana tena imani nao.

Pepe Kavota mkuu kiongozi wa shirika la kiraia Mjini Beni aomba jeshi la Congo na FARDC kuto kubali ushirikiano huo kwani hauna umuhimu kwa sasa.

Olivier Syasemba - AM/MTV News DRC