TANZANIA

Umoja wa Mataifa kupitia MONUSCO nchini DRC yasikitishwa kuhusu mauaji ya waandamani Mjini Goma

SEPTEMBA 1, 2023
Border
news image

Kinshasa, Ogasti 31 2023 ; Tume ya umoja wa mataifa kwajili ya kustawisha amani Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo (Monusco) ina taharifa kwamba kuna Raia wengi walio fariki wakati wa maandamano iliyo pigwa marufuku jijini Goma, Juma tano Ogasti 30 ,2023. Kwa dhamana walio nayo kiusalama Nchini , Idhara za ulinzi nchini Kongo zili jaribu ku zuia kufanywa kwa maandamano hayo , ambayo ina tajwa na baadhi ya waandaaji kwamba ilikuwa kali .

Muwakilishi maalum wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa nchini DRC pia kiongozi wa Monusco Bibi Bintou Keita , asema kusikitika zaidi kwamba maandamano iliyo katazwa ije kusababisha vifo miongoni mwa Raia , askari polisi na askari jeshi wa Kongo na majeraha wengi.

Kwa niaba yake na kwa niaba ya Monusco Bibi Bintou Keita ame towa pole za rambirambi kwa viongozi wa DRC, na jamaa zilizo poteza ndugu zao uku aki watakia majeraha wote uponyaji mwema .

Monusco imesema kuguswa na vitisho pia vitendo vya uhalifu vilivyo shuhudiwa kabla ya maandamano , iki kumbusha umuhimu wa wa kusuluhisha tofauti na mizozo kwa njia ya mazungumzo.

Tume inaendea kupatia moyo viongozi wa Kongo kufungua uchunguzi usio egemea upande wowote , walio fungwa walindwe kulingana na katiba chini ya misingi ya haki za binadamu katiba sheria za kimataifa zilizo ratibiwa Nchini.

Monusco ita endelea kufuatilia hali ya mambo na kutoa mahitaji muhimu kwa viongozi ili kuheshimisha haki za binadamu kwa kutia utaratibu na wafungwa kutendewa haki .

Kwa dakika za mwisho ni kwamba mahakama ya kijeshi imeanza kuwasikiliza watu wanao shukiwa kuwaua na kuwajiruhi wafuasi wa kanisa la wazalendo Mjini Goma.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania