DRC GOMA

UKOSEFU WA USALAMA UNAO SABABISHWA NA WATU WENYE SILAHA WAKISIRI KATIKA MJI WA GOMA KILA SIKU KUKICHA.

Aprili 05, 2024
Border
news image

Hali ya wasiwasi kwa sasa yakumba wakaazi wa Mji wa Goma na kando kando,kufatia ujambazi ,mauaji na wizi wa ngawira ambao umekita miziz katika mji wa Goma . Watu wenye silaha wakiwatwanga risasi na kuwaua watu kila jioni n ahata kupora mali ya watu usiku.

Katika wiki moja watu Zaidi ya nane wakiwa wameuwawa kwakupigwa risasi na watu wasio julikana wakiwa na silaha mikononi katika kata mbali mbali ,.na hata nyuma za watu ziki vaamiwa kwa saa za usiku na kubeba mali ya watu.haya yakijiri katika kata mbali mbali mjini Goma n ahata wilayani nyinragongo.

Nyiragongo ni wilaya inayo pakana na Mji wa Goma ambako kuna kambi. Nyingi za wakimbizi wa ndani walio mkimbia vita kati ya M23 na jeshi la serikali ya Congo FARDC ,wakimbizi wasema milio ya risasi imekuwa ikisika katika kambi zao kila jioni bila kufahamu sababu kubwa.

Kwasasa kuna solaha nyingi Katika Mjini wa Goma ,zikiwa mikoni mwa jeshi,wazalendo na watu wengine ,silaha ambazo kwa sasa ni tishio kwa wakaazi .wachambuzi wa maswala ya kiusalama wakiomba serikali kuchukuwa mikakati Zaidi kuwaweka kambini watu wote wanao miliki silaha.kwani ni vigumu kufahamu nani nina kwa sasa kutokana kwamba kuna watu wasio vaa uniform za jeshi lakini wakiwa na silaha mikoni.

AM/MTV DRC ONLINE