DRC /KAZI ZA UJENZI WA MIONDO MBINU

Serikali ya Congo DRC hasa ya Kivu kaskazini yaanza kazi za ujenzi wa muondombinu hasa ujenzi wa Barabara katika Miji ya Goma, Butembo na Beni.

FEBRUARI 09, 2024
Border
news image

Akizungumuza na wanahabari baada ya sherehe za kuanzisha kazi za ujenzi wa Barabara katika Mji wa BUTEMBO KIVU KASKAZINI naibu Gavana wa Kivu Kaskazini aliwasikli mujini Butembo Romy Ekuka amesema serikali ya Congo kwa sasa imeamua kuanzia kazi za maendeleo chini yaani kwenye wilaya na Miji kama njia moja ya kukuza maendeleo na kufikia wakaazi wa chini.Mjini Butembo nikilometa tatu kujenga barabara Nyamwisi kunako njia panda ya Concorde.

Naibu Gavana Romy Ekuka Lipopo alisema kwamba ukarabati huu ni mwanzo wa muradi mkubwa wa kuboresha Miji mbali mbali Kivu kaskazini

Directa mkuu jimboni wa OVD upande wake, alisema barabara hiyo itakuwa ya urefu wa kilometa 3 yaani toka njia panda la Concorde mupaka uwanja wa ndege wa Rughenda. Bwana Timothée Sumaili aliongeza kwamba kazi zitaendeshwa kwa muda wa myezi 12 na zitatumia zaidi ya milioni 7 dola za kimarekani.

tuseme ya kwamba kambuni Jeryson construction ndio itafanya kazi hiyo.

MTV