TANZANIA

Sijaridhishwa na Makisio ya Gharama za Ujenzi- Dkt. Mfaume

FEBRUARI 29, 2024
Border
news image

Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais -TAMISEMI nchini Tanzania Dkt. Rashid Mfaume hajaridhishwa na tabia ya baadhi ya Waandisi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kuandaliwa na kufanyiwa makisio ya gharama za michoro ya huduma na mkandarasi.

Hali hiyo imefanya makadirio ya gharama za ujenzi kuwa kubwa na kuitia hasara Serikari.

Dkt. Mfaume ameyasema hayo alipokuwa akikagua miradi ya ujenzi na huduma zinazotolewa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Arusha

Amesema makadirio hayo huwa yanafanywa na Mhandisi wa Halmashauri na mkandarasi hapaswi kundaa makadrio hayo baada ya kukabithiwa kazi kwa kuwa inaongeza gharama za mradi.

Akikagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje kwenye Kituo cha Afya Levolosi amesema: " inasikitisha kazi ambayo inatakiwa kufanywa na mhandisi inafanywa na mkandarasi, hili halikubaliki ni kosa kisheria."

Kuhusu ujenzi wa jengo hilo, Dkt. Mfaume amesikitishwa na kasi ndogo ya ujenzi wa jengo hilo ambalo lilitengewa fedha mwaka 2022/2023 lakini mpaka leo jengo hilo lipo katika hatua ya msingi.

Pia Mkurugenzi hajafurahishwa na Halmashauri kutokuwa na vikao rasmu na Mkandarasi vya kufuatilia utekelezaji wa mradi kutoka mradi huo uanze, jambo ambalo limechangia mradi kuchukua muda mrefu kukamilika.

Aidha, Dkt. Mfaume amezitaka Timu za usimamizi na uratibu wa shughuli za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii ngazi ya Halmashauri (CHMT) na Mkoa (RHMT) kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa mara kwa mara ili kuhakikisha.

Kituo cha afya Levolosi kimepokea shilingi milioni 642 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 500 ni fedha toka Serikali kuu na shilingi milioni 142 ni fedha za mapato ya ndani.

MTV Tanzania