DRC - BUTEMBO

Shughuli za kibiashara zimesimamishwa leo Butembo, Kivu Kaskazini, Congo, kutokana na mgomo wa nyumbani ulioitishwa na mashirika ya kiraia kuungana na familia za wahanga wa mauaji yanayodhaniwa kufanywa na ADF

JUNI 18, 2024
Border
news image

Shughuli za kibiashara zimesimamishwa tangu asubui ya leo Katika Mji wa Butembo Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo ambako mashirika ya kiraia iliomba mgomo wakubaki nyumbani kama halama ya kuungana na familia za watu walio poteza ndugu zao kutokana na mauaji inayo endelea kutekelezwa na watu wenye silaha wanao dhaniwa kuwa ADF.

Tangu asubui duka zimeonekana zikifunga milango yake wafanya biashara wamoja wakisimama kwenye milango yao kutazama hali ya kiusalama ,Pamoja na Benki kufunga baada ya mwito wa wakaazi kulalamikia kile wanacho kiita mauaji ya kimbari inayo tekelezwa dhidi yao na watu wanao jiita kuwa ADF.mauaji ya Beni kwa sasa ikiendelea katika Mji wa Lubero ambako katika wiki moja na nusu watu Zaidi ya (200) miambili wameuwawa kwa mapanga ,visu,shoka kukatwa vichwa na watu wenye silaha wakivaa ,kama wakaazi na wengine kama wanajeshi .

Idadi kubwa ya watu walio uliwawa ikiwa kwenye vijiji vya Masala,Kabweke,Maindoni,Keme,Makusa,Masau ,Mantumbu,Masana,Mangano karibu na Mji wa Kantine ambako mili ya watu wengi imezikwa,wakaazi wakisema wengine ambao idadi yao haijulikane walitekwa na kupelekwa sehemu isio julikana .mauaji ikielekea wilayani Lubero eneo la Kambau ambako watu Zaidi ya thelathini wameuwawa kwatika wiki moja na kusababisha maelfu ya watu kutoroka vijiji vyao.

Beni imeshuhudia mauaji kwa Zaidi ya miaka kumi hadi sasa ,katika uangalizi wa Umoja wa Mataifa MONUSCO na sedeke ,japo umoja wa Mataifa umekuja DRC katika ulinzi wa Raia vikosi hivyo vimeonekeana kushindwa kurejesha usalama kwenye vijiji ,kwani eneo wanazo patikani bado hali inaendelea kuwa mbaya na watu kuwawa kila siku.

Wakaazi wa Beni na Lubero na sehemu moja ya Ituri wakiomba usalama na jeshi la Congo FARDC kupewa vifaa Zaidi kwakupiganisha watu wanao husika na mauaji ambayo imesababisha vifo vya watu Zaidi ya Elfu Kumi hadi sasa.

AM/MTV News DRC