DRC TANGANYIKA

SHIRIKA LA MADINI MATA FOREST JIMBONI TANGANYIKA LASIMAMISHWA KAZI NA LIWALI WA JIMBO HILO ...

JANUARI 30, 2024
Border
news image

Shirika hilo la madini linalo endesha kazi zake jimboni Tanganyika, limesimamishwa kazi zake za kuchimba gume gume na muchanga kunako kituo cha uchimbazi wa muchanga eneo hilo.

Hiyo ni kupitiya waraka iliyo sahiniwa na kutangazwa naye liwali wa jimbo la Tanganyika, juma mosi tarehe tatu February elfu mbili ishirini na ine akishutumu shirika hilo kuto kuwa kwa usawa na kodi mbali mbali za serekali ya jimbo hilo. Viongozi hawa waripoti ya kwamba, shirika hilo haliheshimu kanuni za uchimbazi madini inchini DRC, ndio maana wali lishimamisha kazi.

Kwa upande wa shirika Mata Forest, viongozi wa shirika hilo waliweza kumuonesha dhahiri vikartasi mbali mbali vinavio waruhusu kuendesha kazi zao katika eneo hilo.

Kufwatana na hatua yake liwali ambayo kiongozi wa shirika Mata Forest hakuweza arifiwa kabla kuitekeleza, walishangaa kuona kwamba kituo hicho cha uchimbazi gume gume kimezingirwa na askari polisi walinzi wahusikao na mambo ya madini. Kufwatana na hali hiyo, kazi za ujenzi wa daraja kunako barabara ya taifa nambari tano zilizo kuwa zi ki endeshwa na shirika hilo zime simamishwa. Jambo ambalo hali wafurahishe wakaaji eneo hilo wakiomba serekali jimboni kushirikiyana na shirika hilo kwani laendelea kutumika kwa maslahi ya wakaaji. Jambo hilo litaweza chunguzwa mara ingine kabla ya kuwa izinisha kuendeleza kazi zao eneo hilo. Image site Groupe Forest international

NDIWELUVULA BIN MUTUME MTV NEWS Online