DRC

Shirika la Kutetea haki za binadamu barani Afrika ASADHO lahofia muundo wa kesi kuhusu wahusika wa mauaji Mjini Goma Kivu Kaskazini

SEPTEMBA 6, 2023
Border
news image

Mwana sheria Jean-Claude Katende, Msimamizi wa ASADHO Shirika lenyi kutetea haki za binadamu barani Afrika (ASADHO) asema kuwa ana wasiwasi kuhusu hali ya mauwaji ya raïa iliyo enedeshwa Mjini Goma, Kivu Kaskazini ogasti 30, 2023, mashariki mwa DRC. hususane wakati wa maandamano ilio pangwa na dini ya Wazalendo. Serekali ya Kongo ilitangaza vifo vya watu zaidi ya arubaini waliofariki, zaidi ya hamsini kujeruhiwa na zaidi ya miamoja hamsini kukamatwa. Vyombo vya usalama vimetajwa kuhusika na mauaji haya yaliyotekelezwa katika eneo la Nyabushongo pa Ndosho magharibi mwa Mji wa Goma.

Miongoni mwa vikosi vilivyo shutumiwa katika mauwaji ni pamoja na Walinzi wa Raïs (GR), na polisi wa taifa la Kongo. Kwa mujibu wa shirika ASADHO, kuwepo kwa walinzi wa Raïs kwenye eneo la mkasa kunazua maswali kadhaa.

“Kusema kweli, ni lazima niwaambie kwamba ukandamizaji huo ulinisikitisha sana, ikumbukwe kwamba Askari wa ulinzi wa Raïs walikuwa mahali ambapo si sehemu ya kazi yao. Kwa sababu uhudumishaji wa utulivu na urejeshaji wa utulivu kikatiba ni jukumu la polisi wa kitaifa wa Kongo. Lakini hapa Jeshi la ulizi wa Raïs ulifanya shughuli ambazo si sehemu ya dhamira yake, ni muhimu tujue ni nani aliyetoa amri kwa Askari hawa kufanya jambo hilo kwani kazi yao ni kumlinda Raïs wa Jamhuri, wanafamilia wake na mali zao," alisema Mwana sheria Jean-Claude Katende, Msimamizi wa shirika ASADHO.

Shirika ASADHO ya zani ya kama, Felix Tshisekedi lazima athibitishe kwa wananchi dhamira yake ya kutenda haki, hasa kwa vile ni jambo lisilokubalika kwa kitengo cha Kongo kutumwa kuwaua Wakongo ambao hata hawakuwa kwenye barabara kuu ya umma. Anaamini kwamba uchunguzi usio na upande wowowte lazima ufanyike kwa haraka.

Serikali ya Kongo ilitumatimu la mawaziri kutoka Mji mkuu wa Kinshasa hadi Goma Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Ndani, Naibu waziri mkuu wa Ulinzi, Waziri wa Sheria na Waziri wa Haki za Binadamu, akiandamana na mkaguzi mkuu wa kijeshi. Kwa saa 48, ujumbe huu ulifanya mashauriano na idadi ya watu ili kuelewa hali hiyo.

Mahakama ya Kijeshi ya Goma imeanza kesi ya mauaji ya Agosti 30 Mjini Goma. wanajeshi 6 ndio wakiwa ndio wamefikishwa mahakamani , wakiwemo maafisa wawili wa ngazi za juu wa jeshi la FARDC ( GR).

Asaph Litimire