Baada ya kikao cha mawaziri wakuu wa Mikoa hatua kali za chukuliwa kwa wamiliki wa Boti na meli ziwani Kivu ,serikali ime mkamata mmiliki wa Meli ilio zaman a kuwawaua watu Zaidi ya miamoja katika ziwa kivu mashariki mwa Congo ,serikali inasema mumiliki wa meli hiyo ni miongoni mwa walio changia kufanyika kwa ajali Pamoja na wafanya kazi kwani hawakuzingatia sheria za usahafirishaji ziwani.
Wakaazi wa Mikoa ya Kivu Kaskazini na kusini wakiwa bado wana vunja machozi baada ya ajali hii nalkuomba serikali kufungua barabara Goma Minova kwani ni chanzo cha Boti na meli kubeba mizigo ya kupindukia kwa sasa na kusababisha ajali nyingi .
Baadhi ya familia zasema hadi sasa hawajapata ndugu zao ambao wanaripotika kukwama ndani ya Meli hiyo ilio kuwa ikitoka minova kuja Goma na kuzama dakika chache kabla ya kuwasili kwenye bandari ndogo Serikali ya Jamhuri, ambayo ilituma ujumbe kwenye eneo hilo, kutazama namana ya kufanya juhudi za kupata mili ilio kwamba bila mafanikio kwaa sasa .
Kwa sasa serikali yaendelea kutangaza vifo vya watu ishirini na nane na wengine Zaidi ya hamsini kuwa ndio waliokolewa lakini wakaazi wasema walipoteza watu Zaidi y amia tatu wote ambao hadi sasa hawaja patikana na juhudu za kufikia meli hiyo zikiwa ngumu kukiwa hakuna tena Imani yakupatikana kwa watu walio hayi.