Tanzania

Serikali Ya Tanzania Inatekeleza Mradi Wa Umeme Utakaounganisha Tanzania Na Zambia

JULAI 30, 2024
Border
news image

Serikali imesema kuwa mradi mkubwa wa usafirishaji umeme wa TAZA unaohusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha Tanzania na Zambia (TAZA) pamoja na vituo vya kupoza umeme vya Tagamenda, Kisada, Iganjo,Nkengamo na Malangali utawezesha kuunganisha Bara la Afrika kwa nishati ya umeme kutoka Afrika Kusini hadi Ethiopia.

Hayo yameelezwa Mjini Sumbawanga mkoani Rukwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko wakatiakiweka jiwe la msingi la utekelezaji wa mradi huo mkubwa wausafirishaji umeme ambao unahusisha kipande cha kilomita 4 kutoka Tunduma hadi Nakonde mpakani mwaTanzania na Zambia.

Ametaja miradi mingine inayotekelezwa kuwa ni wa umeme Jua wa Kishapu(MW 150), Malagarasi (MW 49.5) na ya GesiAsilia huku lengo likiwa nikuwa na uhakika wa umeme wa kutosha.

Pamoja na utekelezaji wa miradi hiyo, Dkt. Biteko amesema uzalishaji wa umeme lazima uende pamoja na kazi yauungashiaji umeme wananchi kupitia miradi mbalimbali kamawa TAZA ambao unawahakikishia Wanarukwa upatikanaji wa umeme wa gridi ambao utakuwa wa uhakika na wa kutosha.

Amesema kwa sasa Mkoa wa Rukwa unapata umeme kwa kiasi kikubwa kutoka nchini Zambia kwa gharama ya shilingi bilioni 15 kwa mwaka hivyo kukamilika kwa mradi huo kutaifanyaTanzania kuacha kununua umemekutoka nchi hiyo isipokuwa nyakati za dharura.

Ameongeza kuwa, mradi wa TAZA utafaidisha pia maeneo yanayopitiwa na mkuza kutoka mkoani Iringa hadi Rukwa kupitia vituo vya kupoza na kusambaza umeme na kuwezesha kufanyika kwa biashara ya umeme katika nchi zilizopo Mashariki mwa Afrika kupitia Southern African Power Pool (SAPP) na Easten Africa Power Pool (EAPP).

Dkt, Biteko pamoja na kuipongeza TANESCO kwa utendaji mzuri wa kazi, ameiagiza taasisi hiyo kuhakikisha kuwa kasi ya utekelezaji mradi wa TAZA inaendelea kuwa kubwa, na kwamba tukio la kuwekwa kwa jiwe la msingi lisiishie kwenye kupiga picha na kisha kutokomea bali wausimamie mradi huo ili ulete matokeo tarajiwa.

Akigusia usambazaji wa umeme vijijini mkoani Rukwa, Dkt.Biteko amesema kuwa Serikali haifurahishwi na kasi yake ya utekelezaji wa miradi kwani analalamikiwa kusuasua na hivyo ameagiza kuwa ifikapo Agosti mwaka huu awe amemaliza kazi na asipotekeleza agizo hilo achukuliwehatua za kimkataba na hii inajumusha pia wakandarasi wengine wazembeikiwemo katika Mkoa wa Kagera.

Kuhusu utekelezaji wa TAZA, Dkt. Biteko ameshukuru Wafadhili wa mradi huo ambao ni Benki ya Dunia (WB), Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) ambao kwa pamoja wametoa zaidi ya shilingi Trilioni Moja za kutekeleza mradi huo ambao pia unahusisha ujenzi wa vituo vitano vya kupiza umeme. Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inawajali wafadhili wetu.

Kuhusu Nishati Safi ya Kupikia, Dkt. Biteko amesema kuwa Serikali itaendelea kuipa kipaumbele ajenda husika kwani imeshaanzisha Kitengo cha kushughulikia nishati hiyo ndani ya Wizara na kwamba Benki ya Dunia imeahidi kuangalia namna ya kuiwezesha Serikali kutekelezaajenda hiyo.

Kwa upande wake, Katibu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema mradi wa TAZA ni wa kipekee kwa sababu utawezesha Afrika kuunganishwa na umeme kutoka Afrika Kusini hadi Ethiopia.

Naye, Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Luteni Jenerali Mathew Mkingule ameishukuru na kuipongeza Serikali ya Tanzania kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ukiwemo mradi wa umeme wa TAZA ambao amesema utahakikisha usalama wa nishati katika nchi za Kusini mwa Afrika, kukuza uchumi Mkoa wa Rukwa, kuwezesha biashara ya umeme, fursa ya ajira na kulinda mazingira kwani nishati ya umeme inawezeshawananchi kutumia nishati hiyo katika kupikia.

Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Nathan Belete kwa niaba ya Wawekezaji wa mradi amempongeza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko pamoja na Serikali kwa ujumla kwa miongozo ambayo imewezesha mradi wa TAZA kuanza kutekelezwa.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga alieleza kuwa, mradi wa TAZA ni sehemu ya maazimio ya yaliyofanyika tarehe 15 Desemba 2014 baina ya Tanzania, Kenya na Zambia yakuunganisha gridi za nchi hizo tatu.

AM/MTV News DRC