Tanzania

Serikali Ya Tanzania Imewataka Wananchi Kutumia Fursa Ya Siku Za Nyongeza Maonesho Ya Nanenane Kuchunguza Afya Hadi Tarehe 10 Agosti, 2024

AGOSTI 10, 2024
Border
news image

Katika utekelezaji wa Kampeni ya Mtu ni Afya, Wananchi wameaswa kutumia fursa siku za nyogeza maoenesho ya nanenane Kitaifa kupata huduma za afya ikiwa ni pamoja na kuchunguza kupitia vipimo mbalimbali ikiwemo vipimo vya macho, homa ya Ini .

Hayo yamebainishwa leo Agosti 8, 2024 na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya Dkt. Ona Machangu katika Maonesho ya Wakulima Nanenane Jijini Dodoma ambapo ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kujitokeza katika banda la Wizara ya Afya kupata Huduma mbalimbali ikiwemo Elimu ya Afya , huduma za macho na Homa ya Ini.

“Zipo huduma mbalimbali katika banda la Wizara ya Afya ikiwemo upimaji wa Homa ya Ini na chanjo , Uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi, Saratani ya Matiti, Kifua Kikuu, Virusi vya UKIMWI,elimu ya afya kuhusu afya ya akili, mazoezi, Malaria , bima ya Afya , lishe ,Tiba Asili na huduma nyinginezo nyingi hivyo nitoe wito kwa Wananchi hususan Dodoma na mikoa jirani kuendelea kujitokeza kupata huduma bora za afya Nzunguni Dodoma hadi Agosti 10,2024”

Aidha, Dkt. Machangu amehimiza jamii kuendelea kuzingatia mlo bora na umuhimu wa kufanya mazoezi katika kuimarisha Kinga ya Mwili.

“Tunatekeleza Kampeni ya Mtu ni Afya ,Fanya kweli Usibaki nyuma miongoni mwa vipaumbele ni kuzigatia mlo bora na mazoezi kuimarisha afya pia kufanya usafi wa mazingira yanayotuzunguka”amesema.

AM/MTV News Tanzania