DRC

Serikali ya Kivu kaskazini yawachukulia hatua viongozi wa uchukuzi kwenye bandari baada ya ajali ya Meli katika ziwa Kivu

OKTOBA 03, 2024
Border
news image

Akizungumuza na MTV Isac mmoja wa walio nusurika kifo baada ya kuokolewa na wavuvi asema hali ilikuwa mbaya na meli yao ilikuwa ikibeba watu wengi na mizigo ya kupindukia ndio chanzo cha ajali ya meli .

Isac amesema meli yao ilikuwa ikibeba watu Zaidi y amia tatu na walio nusurika ni wachache ila wengi walizama Pamoja na Meli hiyo.

Miongoni mwa walio fariki Mtoto mchanga alie fariki Dunia na mamae baada ya kuokolewa dakika chache.meli ilio kuwa ikitoka katika mji wa Minova Kivu kusini ilizama katika ziwa Kivu ilipokuwa ikiwasili kwenye bandari ndogo la Kitu katika Mji wa Goma.ma mia ya abiria wengi walikuwa ni wakaazi wa wilaya ya kalehe na vijiji vingine ambao wlaikuwa wakiekea Mjini Goma kwa shughuli za biashara na wengine kusalimia familia kwa bahati mbaya wengi wamepotea ziwanai.

Ajali kama hizi hutokea mara kwa mara katika ziwa Kivu boti za vyakula kuzama maji.serkali ya Kivu kaskazini imemsimamisha kazi mkuu wa uchukuzi kwenye bandari kutokana na kuto heshimi sheria za usafiri majini ,hadi sasa mili mingine ikiwa haijapatikana na meli hiyo ikiripotika kuwa kwenye umbali wa meta miamoja arbaini ndani ya ziwa .

Vilio vikishuhudiwa kila sehemu mjini Goma na wilayani Kalehe ambao wengi walitokea .

AM/MTV News DRC