DRC

DRC serikali ya DRC yatangaza kuwakamata baadhi ya makaamanda walio husika katika mauaji ya raia wazalendo Mjini Goma tarehe thelathini iliopita

SEPTEMBA 5, 2023
Border
news image

Akizungumuza na wanahabari katika Mji wa Goma,Piter Kazadi Kankonde Waziri wa mambo ya ndani wa Congo DRC asema kamata ilio tumwa na Rais FELIX Tshisekedi imemkamata kamanda mmoja wa GR ambae ni miongoni mwa watu walio husika katika mauaji ya raia walio kuwa wakiandaa maandamano ya kupinga MONUSCO tarehe thelethini iliopita.waziri Kazadi ameongeza kuomba kwa wakaazi wa Mji wa Goma kuwa watulivu kwani mahakama ya kijeshi kwa sasa itaanza kusikiliza kesi ya watu wote walio husika kwa mbali ama kwa karibu katika ukiukwaji wa haki za binaadamu Pamoja na vurugu ambazo zimepelekea uhusiano kati ya jeshi la serikali ya wananchi kuelekea njia mrama.

Hadi sasa kamati ya timu la mawaziri nne kutoka Kinshasa bado inaendelea kuwasikiliza watu mbali mbali ambao waliathirika kwa mbali ama kwa karibu katika shambulizi lilo tekelezwa na jeshi tiifu kwa serikali ya Congo.mkuu wa kanisa la wazalendo Ephrem Bisimwa akiwa tayari mikononi mwa Vyombo vya usalama.

AM/MTVNEWS