DRC

Serikali ya Congo yaomba Umoja wa Africa kusima na kuchukuwa hatua kwa ajili ya suluhisho kuhusu Mzozo mashariki mwa DRC

DISEMBA 08, 2024
Border
news image

Wakiongozwa na mheshimiwa Timoléon Baikoua, rais wa kundi la wabunge na makamu wa rais wa kamati ya ushirikiano wa kimataifa na utatuzi wa migogoro katika bunge la Pan-Afrika, katika nchi 7 wanachama wa ujumbe wa Umoja wa Afrika wametembelea Mji wa Goma kuchunguza hali iliyopo mashariki mwa DRC.

Wabunge hao ikiwa ni kutoka taifa la Ghana, RSA, Djibouti, Sudan Kusini, Somalia, Benin, DRC. Wajumbe hao Walizungumza na kamati ya usalama ya mkoa inayoongozwa na Gavana kwa muda wa Kivu Kaskazini, mkuu wa ofisi ya MONUSCO Kivu Kaskazini, rais wa bunge la mkoa, wa wakilishi wa maungamo ya kidini, asasi za kiraia, vijana pamoja na wanachama wa mashirika ya wanawake.

Baada ya mikutano hii, wajumbe hao walikwenda katika moja ya maeneo ya watu waliokimbia makazi yao yaliyo karibu na jiji la Goma yaani wakimbizi wa Ndani.

Baada ya ziara hii ujumbe wa Bunge la Africa wasema watatembelea mataifa jirani ya Congo kuwahamasisha kuacha uvaamizi wa Taifa huru la DRC. Wabunge hao wasema mali ya Congo ndio chanzo cha mateso ya raia na uvaamizi wa ardhi ya DRC. Umoja wa Africa ukishutumiwa kushindwa kuchukuwa hatua kwa ajili ya mzozo wa Mashariki mwa Congo.

AM/MTV News DRC