DRC

Serikali mpya yaapishwa na Bunge la DRC

JUNI 11, 2024
Border
news image

Judith Suminwa Tuluka ndie Waziri mkuu wa serikali ya Congo DRC ,serikali ambayo itakabiliana na changa moto kubwa kutokana na uasi wa M23 mashariki mwa Congo Pamoja na swala la ADF ambao kwa sasa washutumiwa wote kuendesha vitando vya ukiukwaji wa haki za binaadamu.

Suminwa amesema serikali yake kwa sasa itajikita katika swala la usalama mashariki mwa Congo Pamoja na tatizo kubwa la wakimbizi wa ndani wanao kimbia vita vinavyo enedelea kati ya M23 na jeshi la serikali kutoka wilaya ya Masisi,Rutshuru,Nyirago na lubero kwa sasa ambako M23 imekuwa iki vurumisha mabomu kwa wakaaazi.

Judith Tuluka asema serikali yake itajitahidi kuwapa vijana ajira na kuwalinda wananchi wa Congo ili wafaidike kwa raslimali ya ndani ,Congo nintaifa lenye utajiri mkubwa lakini utajiri ambao wananchi wake hawafaidiki hada kidogo ,hasa madini yake ikiibwa kila siku na mataifa Jirani ,wanasiasa na mataifa yenye nguvu Duniani na wkaazi wakibaki fukura.

Judithi amesema hali mashariki mwa Congo ni mbaya kutokana na na uasi wa M23 ,swala ukosefu wa usalama Mkoani Ituri,Maniema na Kivu Kusini .eneo la Kasai na Katanga kukiwa migogoro ya kikabila .

Uchumi wa Congo umekuwa uchumi ambao unadidimia kila siku .wakaazi mikoa mbali mbali ya DRC wakiomba amani na usalama na kuboresha miuondombinu hasa ujenzi wa barabara muhimu kwakuunganisha mikoa ambayo nivigumu kufikia.

Usafiri katika taifa la Congo umekuwa tatizo kubwa kwa wananchi wake huku wenye pesa wakitumia ndege kama njia bora kwa ushafirishaji wa watu na mali.

Serikali ya Suminwa inahitajika kuwajibika kwa ajili ya ombi muhimu la wananchi ,usalama,maendeleo na afia.

AM/MTV News DRC