DRC

Serikali kivu Kaskazini yaomba wakaazi katika eneo la Bweremana na Minova kuunga mkono Juhudi za Maendeleo zinazo tekelezwa kwa sasa

SEPTEMBA 02, 2024
Border
news image

Akizungumuza na wakaazi wakati wa kuanzisha Kazi za ujenzi wa daraja Renga katika Kijiji cha Bweremana wilayani Masisi Meja Generali Peter Cirimwami gavana wa Kivu kaskazini asema ujenzi wa daraja Renga ni muhimu kwa ushafirishaji wa bidhaa na vyakula kwa wakulima Pamoja na wasafiri kutoka kivu Kaskazini kwenda kivu Kusini .

Pamoja na hali ya kiusalama eneo hilo Cirimwami alisema serikali kwa sasa yafanya liwezalo kuhakikisha usalama wa wakaazi unapatikana na barabara Minova Goma inafunguliwa kwakupisha uhuru wa wakaazi kutembea kwenye vijiji vyao.wakaazi eneo la Bweremana na Minova wakilaumu serikali kushindwa kuwaondoa waasi wa M23 kwenye milima ikiwa ni mashamba yao .

Hali inayo sababisha uchumi kudidimia na hali ya Maisha kuwa Ngumu Zaidi akisema Mwami Kalinda Kibandja Nicolas mkuu wa eneo la Bahunde .wakaazi wakiomba serikali kuhudumisha usalama kwa haraka kwaani hali wanayo pitia ni ngumu na mbaya Zaidi .

Gavana Cirimwami asema lazima maendeleo ishughulikiwe japo kuna matatizo ya kivita ila hivi karibuni suluhu litapatikana.

AM/MTV News DRC