DRC BENI

Seneta Papy Machozi awetembelea wakaazi wanao kimbia vijiji vyao kutokana na kushambuliwa na ADF

SEPTEMBA 12, 2024
Border
news image

Akiwa na mzigo mkubwa wa vyakula mbali mbali Seneta Papy Machozi amekutana na wakaazi watu waliokimbia makazi yao kutokana na vita vya kigaidi vya ADF ambao hushambulia wakaazi mara kwa mara .Seneta Papy Machozi amewatembelea wakaazi ambao wengi wamesha poteza makaazi yao na jamaa na marafiki .Machozi amewalekea msaada wa Chakula mamia ya watu waliokimbia makazi yao katika eneo la Luvangira Oïcha, seli , wilayani Beni, Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo DRC Jumatano Septemba 11, 2024.

Machozi alisema hii ni Pamoja na kuungana na wakaazi wanao pitia magumu ya kikatili inayo tekelezwa na ADF kwa muda mrefu.

Msaada huo ulihusisha vyakula vikiwemo mchele, maharage, unga na vingine. Machozi ni Seneta mzaliwa eneo la Beni na sehemo ya familia zake wengi wakiwa wamesha poteza Maisha katika maujai hayo.

Machozi alisema wakaazi hao wana hitaji kubwa hasa usalama ,Pamoja na huduma nyingine muhimu na haraka kwani wakaazi wengi sasa wamebaki masiki baada ya mashamba yao kuwa misitu baada ya kuhamishwa kwa nguvu. Watu wengi waliokimbia makazi yao wameomba Seneta Papy Machozi kuwa mtetezi wao kwa viongozi wa serikali kuu ya Kinshasa ili kuhudumisha amani na usalama kwani lengo kubwa nikuona wanarudi kwenye mashamba yao.

Muda mfupi kabla ya kukabidhi msaada kwa waliofurushwa makwao, Seneta Papy Machozi alizungumza na naibu msimamizi wa eneo la Beni. Watu hao wawili walishughulikia masuala kadhaa ya maslahi ya jamii. Na zaidi hasa changamoto zinazokabili eneo la Beni zinazo sababisha usalama mdogo kwa muda mrefu.

George Musubaho /MTV News DRC