DRC

SADC yaamua kuondoa wanajeshi wao mashariki mwa Congo wakati bado waasi waandelea kuteka maeneo yaani vijiji na miji kadhaa mkoani Kivu Kaskazini kama vile Kivu Kusini

MACHI 16, 2025
Border
news image

Baada ya kikao cha viongozi wa SADC kufanyika, Jumhia hiyo imeweka nanga kwa operesheni zake za SAMIDRC operesheni ambazo lengo lake ilikuwa na kutokomeza makundi ya waasi mashariki mwa Congo DRC hasa lile la M23 ambalo ndilo lenye nguvu Zaidi kuliko mengine mengi Zaidi ya mia mbili inayo kuwa na silaha Kivu Kaskazini na Kivu Kusini.

Hatua hii ina jira baada ya waasi waa M23 kuchukuwa mji wa Goma na Bukavu amabko vikosi hivyo vya patikana, hasa katika uwanja wa ndege wa Goma na Mubambiro katika mji wa SAKE magharibi mwa mji mkuu wa Kivu Kaskazini. SADC imepoteza wanajeshi wengi tangu mapigano ya jeshi la serikali na waasi wa M23 ambao Umoja wa Mataifa na ripoti nyingine zasema wanaungwa Mkono na serikali ya Kigali Rwanda.

Wakati wa mapigano ya Goma SAMIRDC ilipata pigo wakati pale wanajeshi wake Zaidi ya kumi na tano walifariki Dunia na wengine Zaidi ya ishirini kujeruhiwa katika uwanja wa Goma na wengine katika eneo la Mubambiro ambako mapigano yalikuwa makali Zaidi.

SADC imekuwa ikisema kuwa waasi wa AF/M23 wame waweka kando wakishindwa kutembea Mjini Goma, yaani wakiwa hawa uhuru. Wakaazi wa Mji wa Goma wakisema SADC imeshindwa kazi zake za kutekeleza amani na usalama kwa nguvu na wengine wakisema SADC imechukua hatua nzuri kuondoka DRC kwani mzozo wa DRC hauwezi tatuliwa kwa silaha lazima kwa mazungumuzo kwani ndio njia bora.

Serikali ya DRC ilitegemea sana vikosi hivi lakini kwa bahati mbaya vimeshindwa kutokana na jeshi la Congo kushindwa kujijenga na kukiwa muingiliano katika jeshi hilo la Congo FARDC. Wanajeshi wengi wengi wa SADC washutumu wanajeshi wengi wa Congo FARDC kuwa upande wa waasi na huwa ndio husababisha operesheni za kijeshi kuwa ngumu.

AM/MTV News DRC