Rais William Ruto amefanya mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri, katika hatua iliyoshuhudia wizara mbalimbali zikiunganishwa na kubadilishwa jina.
Katika hatua hiyo, Rais Ruto alipanua Ofisi ya Waziri Mkuu na kujumuisha Wizara ya Mambo ya Nje na Masuala ya Diaspora, inayoongozwa na Musalia Mudavadi.
Moses Kuria amehamishwa kutoka wizara ya Biashara hadi Wizara ya Utumishi wa Umma, Utendaji na Usimamizi wa Uwasilishaji.Alfred Mutua, kwa upande mwingine, anaondoka katika wizara ya Mashauri ya Kigeni kuongoza wizara ya Utalii na Wanyamapori.Waziri wa Jumuiya ya Afrika mashariki Rebecca Miano kwa upande wake amehamishwa hadi kwenye wizara ya Biashara na Viwanda kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mbunge wa Gatundu Kusini.
Waziri wa Maji Alice Wahome amebadilisha nyadhifa zake na Zachary Njeru wa Wizara ya Ardhi, Kazi za Umma na Maendeleo ya Miji.