ANGOLA

Rais wa DRC Félix Tshisekedi awasili asubuhi ya leo Lobito Angola , katika jimbo la Angola la Benguela kwa siku ya kihistoria iliyowekwa kwa ukanda wa Lobito.

DISEMBA 04, 2024
Border
news image

Mkuu wa Nchi atashiriki wakati wa mchana katika mkutano wa kimataifa kuhusu mradi huu shirikishi pamoja na wenzake Joâo Lourenço wa Angola, Hakainde Hichilema Hichilema wa #Zambia, Makamu wa Rais wa Tanzania na Rais Joe Biden kutoka #Marekani.

Mkutano huu wa kimataifa kuzunguka "Lobito Corridor" unalenga kuhuisha mradi huu wa kimkakati unaoungwa mkono na #Marekani na ambao unajumuisha kuunganisha Bahari ya Atlantiki na Bahari ya Hindi kupitia #DRC. Kando ya ziara hii ya kikazi, Rais Félix Tshisekedi pia anatarajiwa kukutana ana kwa ana na mwenzake wa Marekani Joe Biden, ambaye aliwasili kwa mara ya kwanza barani Afrika.

Rais wa DRC amefanya ziara hii wakati taifa lake laandamwa na mauaji ya ADF wilayani Beni na M23 wilayani Lubero, Masisi na Rutshuru Kivu Kaskazini mashariki mwa Taifa lake.

AM/MTV News DRC