DRC

Rais wa Congo Felix Tshisekedi atangaza kuendelea kuimarisha uhusiano wake wa kijeshi na Uganda

OKTOBA 13, 2024
Border
news image

Mkuu wa Nchi alimpokea Jean-Jacques Bouya, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mipango ya Kieneo wa Jamhuri ya Kongo, ambaye alibeba ujumbe maalum kutoka kwa Rais Denis Sassou Nguesso.

Baadaye jioni, Rais FĂ©lix Tshisekedi alipokea ujumbe kutoka Ungozi wa Jeshi la Nchi Kavu la wananchi wa Uganda. UPDF ambao kwa sasa wanashirikiana na jeshi la Congo katika msakao wa wapiganaji wa ADF katika misitu ya Beni na Ituri mashariki mwa taifa la DRC.

Maafisa hawa wa Uganda waliongozwa na Mkuu wa Majeshi wa Fardc, Jenerali Christian Tshiwewe.

Baada ya kufuatilia ripoti ya operesheni za pamoja dhidi ya shughuli za ADF katika jimbo la Ituri, Rais Tshisekedi alitoa maagizo ya wazi ya kuimarishwa kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Uganda ili kutokomeza ukosefu wa usalama katika eneo hili.

Katika ujumbe huo wali hudhuria mkuu wa operesheni Generali Shiko nae Bruno Mandevu ambao kwa sasa wamekuwa wakiongoza Opresheni za kijeshi katika eneo la Beni kupambana na kuwasaka wapiganaji wa ADF ambao wanashutumiwa kuhusika katika uhalifu na mauaji ya watu wilayani Beni na sehemu Moja ya Ituri.

Mwezi huu wakaazi wa Mji wa Beni walikumbuka miaka kumi tangu mauaji yaanze wilayani Beni ,maelfu ya watu wakiendelea kuwawa kila siku na wengine kutekwa na wapiganaji musituni,katika uangalizi wa Umoja wa Matiafa kupitia MONUSCO ambao wako DRC kulinda raia wa DRC dhidi ya mauaji.

Mauaji yalio anza Beni kwa sasa imezagaa hadi wilayani Jirani ya Lubero kivu Kaskazini na Mambasa Mkoani Ituri .

AM/MTV News DRC