KINSHASA

Rais wa Congo Félix Tshisekedi aongoza hafla ya kufunga toleo la 2 la Jukwaa la Uhandisi wa Kisayansi la Kongo

AGOSTI 30, 2024
Border
news image

Rais wa Jamhuri hii alhamisi alitembelea viwanja vya watafiti katika technolojia , kabla ya kukabidhi nishani kwa washindi

Katika hafla hii, Mkuu wa Nchi alimwagiza Waziri wa Utafiti na sayansi na Ubunifu wa Teknolojia "kuwasilisha, kwa Baraza la Mawaziri, maandishi ya sheria ambayo yatahakikisha ufadhili wa ubunifu na wa kutosha kwa watafiti na wavumbuzi wetu."

Rais Tshisekedi pia aliamurisha serikali "kuunga mkono kwa kiasi kikubwa utafiti wa kisayansi na uvumbuzi wa kiteknolojia, na pia kuzingatia mgao mkubwa zaidi kwa sekta hii katika miaka ijayo. »

Mkutano huu ulilenga kukuza utafiti wa "Made in Congo🇨🇩" na kuhusisha wasomi wa kisayansi wa Kongo katika maendeleo ya nchi yao.

Kati ya miradi zaidi ya 400 kutoka kwa watafiti wanaoishi nchini na nje ya nchi, 50 ilitunukiwa zawadi baada ya uamuzi wa jury.

AM/MTV News DRC