Jumatatu hii katika Ikulu ya Rais ya Mont-ngaliema, Mkuu wa Nchi FĂ©lix Tshisekedi aliongoza mkutano wa Kikosi Kazi cha makamanda wa Kuu wa Kijeshi.
Mkutano huu ukiwa wa pili tangu ulio fanyika Ijumaa Julai 5.
Mbali na Amiri Jeshi Mkuu, mkutano huu uliwakutanisha Naibu Waziri Mkuu anayeshughulikia Ulinzi, Waziri wa Fedha, Amiri Jeshi Mkuu, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na baadhi ya washauri wa Mkuu wa Nchi kufanya tathmini ya jeshi na hali ya usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Katika mkutano huu, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Wanajeshi wa DRC (FARDC) na Polisi wa Kitaifa walifafanua maagizo ya kufuata na kuamuru Kamanda mkuu wa Kijeshi kutekeleza hatua zilizoamuliwa kulinda ardhi yote ya Congo .
Utafahamu kwamba kikao hiki kina jiri baada ya waasi wa M23 kuchujuwa vijiji muhimu wilayani Lubero mashariki mwa Congo ,ikiwemo kanyabayonga,Kayna,Kirumba ,Mighovwe ,Kasewghe ,Miriki na Luofu .Vijiji ambavyo ni muhimu ki stratejia kwa usalama wa Kivu Kaskazini.
Wakaazi wa Miji ya Butembo ,Lubero ,Beni wakiwa kwa wasiwasi kwa sasa kutokana na hali inayoendelea kwasasa.wakaazi wakiishi porini hasa wanawake na watoto .