DRC

Rais wa Congo DRC na wa Burundi wazungumzia swala la usalama mashariki mwa Congo wakiwa China

SEPTEMBA 05, 2024
Border
news image

Baada ya kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa Kongamano la 9 la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC2024), Alhamisi hii mjini #Beijing, Rais Félix Tshisekedi alikuwa na tête-à-tête ya zaidi ya saa moja na mwenzake kutoka #Burundi🇧🇮 Evariste Ndayishimiye.

Viongozi hao wawili wanaodumisha uhusiano wa kindugu walijadili mambo yenye maslahi kwa pamoja, hususan ushirikiano wa nchi mbili na hali ya usalama mashariki mwa #DRC🇨🇩.

Utafahamu kwamba Burundi ina wanajeshi wake mashariki mwaa Congo wakiungana na kikosi cha FARDC katika mapambano yake na waasi wa M23 ambao DRC yasema waungwa Mkono na Rwanda.

AM/MTV News DRC