ZANZIBAR

Rais Samia, Rais Ruto Na Rais Museveni Wakutana Zanzibar

MACHI 14, 2024
Border
news image

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais William Ruto wa Kenya wakiangalia picha ya Viongozi wa Nchi mbalimbali za Afrika wakati Rais Museveni alipomkabidhi Rais Samia zawadi hiyo baada ya mazungumzo yao Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 14 Machi, 2024.

Kwenye mazungumzo yao wamezungumzia masuala ya mtangamano wa Afrika Mashariki hususan umuhimu wa kuharakisha zoezi la kukusanya maoni ya Wananchi Juu ya muundo na maeneo ya kuangaliwa katika Rasimu ya Katiba ya Fungamano la kisiasa la Afrika Mashariki (EAC Political Confederation). Zoezi hilo limeshafanyika katika nchi za Burundi, Uganda na Kenya na linatekelezwa na Timu ya Wataalamu inayoundwa na Wajumbe watatu kutoka kila nchi Mwanachama.

MTV Tanzania