TANZANIA

Rais Mstaafu wa Tanzania Alhaji Hassan Mwinyi Afariki Dunia

FEBRUARI 29, 2024
Border
news image

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Alhaji Ali Hassan Mwinyi kilichotokea leo katika Hospitali ya Mzena iliyopo Jijini Dar es salaa.

Rais Samia amesema Alhaji Mzee Mwinyi amefariki dunia saa 11 jioni ya leo Alhamisi Februari 29, 2024 alipokua akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya mapafu.

"Mzee Ali Hassan Mwinyi, amekuwa akipatiwa matibabu tangu Novemba mwaka jana huko London nchini Uingereza na baadaye kurejea nchini ambapo aliendelea na matibabu katika Hospitali ya Mzena hadi leo umauti ulivyomfika,” amesema Rais Samia.

“Kwa niaba ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania natoa pole kwa familia , ndugu , jamaa, marafiki na watanzania wote kwa msiba huu mkubwa kwa taifa".

Aidha ninatangaza siku 7 za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia kesho.

Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi atazikwa tarehe Pili Machi , 2024 (02.03.2024) huko Unguja Visiwani Zanzibar na taratibu za mazishi zitatangazwa baadae.

MTV Tanzania