Mgogoro wa kiusalama na wa kibinadamu uliopo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), unaoadhimishwa na uwepo wa wanajeshi wa Rwanda wanaowaunga mkono kundi la waasi wa M23, ndio mada kuu katika ajenda ya mkutano huu ulio fanyika kukiwa kuna baki siku chacha kabla ya mkutano wa Angola.
Kwa mjumbe wa Marekani, "uhuru na uadilifu wa eneo la DRC lazima uheshimiwe na wote". "Tutafanya kazi ili kuhakikisha kwamba vikwazo vyote vinavyozuia amani na usalama vinaondolewa ili amani irejee DRC," alihakikishia Bw. Ronny Jackson.
Sambamba na hayo, Mjumbe Maalum wa Rais Trump alielezea matumaini ya kuona uwekezaji wa Marekani ukitua katika ardhi ambayo ina amani na usalama inatawala. “Tunataka kufanya kazi ili makampuni ya Kimarekani kuja kuwekeza na kufanya kazi nchini DRC. Na kwa hilo, lazima tujihakikishie kuwa kuna mazingira ya amani,” alisisitiza Bw. Ronny Jackson.
Mwanachama wa Bunge la Marekani, Bw. Ronny Jackson anafanya kazi katika kamati kadhaa, miongoni mwa zingine kuhusu silaha, kijasusi na uhusiano wa kigeni. Marekani kwa sasa imeomba pande husika katika Mzozo wa mashariki mwa Congo kukaa kwa meza moja na kupata suluhu kuliko kuendelea kupigana.