Baada ya kujadiliana na Dk Jean Kaseya mkurugenzi waAfrica CDC wa Afia Rais Félix Tshisekedi amsema serikali yake kwa sasa imechukuwa hatua ya kupambana na homa kali ya virusi vya Mpox.
Mkuu wa taifa la DRCongo alitangaza kutolewa kwa dola za Marekani milioni 10 ili kuimarisha mapambano dhidi ya janga hilo.
Dk Kaseya alithibitisha kuwasili kwa chanjo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), iliyokusudiwa kwa watu walioathirika, mawasiliano yao na watu walio hatarini.
Waziri wa Afya Dk Roger Kamba alisisitiza kuwepo kwa mpango wa dharura wa kitaifa unaotekelezwa na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Jamii kupitia CRUSP.
"Ni zamu ya mpango huu ambapo serikali imeshirikiana na washirika," aliongeza.
Kuhusu uwezo wa kitaifa wa kusimamia Mpox, Waziri wa Afya alihakikishia kwamba DRC ina utaalamu mkubwa katika udhibiti wa magonjwa na inatoa utaalam huu kwa nchi nyingine.