DRC

Rais Felix Tshisekedi Awasili Harare Kwa Mkutano Wa 44 Wa SADC

AGOSTI 16, 2024
Border
news image

Rais wa Jamhuri Ya Kidemokrasia ya Congo Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo amewasili Harare, Zimbabwe, kushiriki Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC, unaofunguliwa Jumamosi hii. Agosti 17.

Mkutano huu ukiwa na mada: "Kukuza Vipaji kwa nia ya kugundua matarajio mapya ya ukuaji wa uchumi na maendeleo endelevu kwa ajili ya ukuaji wa viwanda wa SADC".

Kabla ya ufunguzi wa mkutano huu, Rais Félix Tshisekedi amealikwa kushiriki katika mkutano wa kilele wa Troika ya Organ ambao unafunguliwa Ijumaa hii mapema jioni.

Rais Tshisekedi atazungumuza mbele ya chombo hicho cha kisiasa kuwasilisha hali ya kisiasa na usalama nchini mwake pamoja na kutumwa kwa Samidrc ambao wako mashariki mwa taifa lake.

Mwishoni mwa mkutano huu wa kilele mjini Harare, Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa atamrithi mwenzake wa Angola Joao Lourenço kama rais wa zamu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Sadc).

AM/MTV News DRC