DRC

Raia wa kabila la wambuti waishio katika kambi ya wakimbizi ilio tengwa kwa ajili yao katika Mji wa Oicha wilayani Beni waomba waomba usalama kwenye mashamba yao ili warudi misituni

SEPTEMBA 13, 2024
Border
news image

Akizungumuza na ujumbe wa wabunge mmoja wa wambuti yaani wabatwa asema mauaji inayo shuhudiwa kwa muda mrefu wilayani Beni imesababisha Maisha yao kuwa mbaya kwani tabia yao sio kuishi Mjini na kwa sasa hali yao ya Maisha ni mbaya wakigon jwa kila siku.

Wambuti ama wabatwa ni watu wanao ishi kwa kuwinda Wanyama pori ,kutafuta matunda na vitu vingine musituni kwa sasa wakiwa hana namna ya kuelekea mashambani kutokana na mauaji inayo tekelezwa na waatu wanao dhaniwa kuwa ADF ambao wamesababisha maelfu ya watu kupoteza Maisha tangu mwa wa elfu mbili na nane haadi sasa wana vijiji wengi wakiuwawa kwa shoka na mapanga.

Maelfu ya watu wamepoteza Maisha kuwawa Mjini Beni,wilayani Beni na wilayani lubero kwa mapanga na shoka na wengi kuwawa kwa visu ,katika uangalizi wa jeshi la serikali ya Congo FARDC,kikosi cha Umoja wa Mataifa MONUSCO ,lakini kwa sasa wakisakwa na jeshi la Uganda UPDF katika ushirikiano wa jeshi la Congo FARDC.

Mbilikimu wamesema wameshangazwa kuona watu kuwawa bila hatia na wengi kulazimika kuhama vijiji vyao na kuwa wakimbizi ,na kwa sasa wakila vyakula ambavyo si nzuri kwa afia yao.

AM/MTV News DRC