DRC GOMA

POLISI KATIKA MJI WA GOMA YAANZA MSAKO WA MAGARI YOTE INAYO KUWA VIYOO VYENYE RANGI NYEUSI VILIVYO PIGWA MARUFUKU NA GAVANA WA MKOA WA KIVU KASKAZINI .

news image

Hatua ya kupiga marufuko kuzunguuka barabarani Mjini Goma kwa magari ambayo ina viyoo vilivyo na rangi nyeusi, ilichukuliwa na viongozi wa mji wa Goma kwa ajili ya kupambana na ujambazi, uhalifu pamoja na bidhaa hararu inayo fichwa ndani ya magari hayo. Utafahamu kwamba, ni magari ya aina hiyo maarufu ya vitre fume ndiyo yawachukua majambazi na kupitisha bidhaa na vitu vibaya ambavio vimepigwa marufuko na serikali.

Kufwatana na hatua hiyo ambayo imechukuliwa na viongozi wa mji wa Goma wakishirikiana na viongozi wa Mkoa , askari polisi wa taifa la Kongo na vyombo vya usalama wame amurishwa kuendesha msako kote Mjini na kuwakamata watu wote wanao kaidi Amri ya Serikali

Na yeyote atakaye kamatwa akitembeza gari ambayo viyoo viake vimetiwa rangi nyeuzi yaani rangi bandia nyeusi ataazibiwa vikali na serekali , Kwaku kaidi amri ya serikali Gvana wa Kivu Kaskazini alipo zungumuza na MTV DRCONLINE alisema magari mengi ya vio vyeusi kwa sasa inatumiwa na majambazi n ahata kuwateka watu Mjini kwa saa za Mchana..

NDIWELUVULA BIN MUTUME MTV NEWS Online