Yshaligonza ametembelea Mji wa Bunia mkoani ituri wakati kumekuwa siwasi kubwa na kufatia twitter za mkuu wa jeshi la Uganda kutishia usalama wa Congo DRC. UPDF kienelea kutundika jeshi lake wilayani Djugu ambako wapambana na wappiganaji wa CODECO wanao ombwa kusalimisha silaha zao.
Ychaligonza ameomba wakaazi wa Mji wa Bunia na wakaazi wote wa mkoa wa Ituri kuwa watulivu, pamoja na kuomba makundi yote ya wapiganaji kusalamisha silaha kwani Ituri haina lazima ya kuwa na wazalendo njia moja nikusalimisha silaha kwa haraka. UPDF yaani jeshi la Uganda limesema kuwa lengo lao kubwa nikushirikiana na jeshi la Congo FARDC. Kuyapokoanya silaha makundi yote yenye silaha.
Ychaligonza amesema Ituri haina lazima ya kuwa na wapiganaji waazalendo kwani wanao kupigana na M23 wako Kivu Kaskazini na Kivu Kusini ambako kuna changamoto ya usalama. Kundi la CODECO kwa upande wake likisema kuwa lita pambana na UPDF iwapo wataendelea kuwashambulia, huku mapigano ya kiripotiwa kwenye baadhi ya vijiji na kuwa watakao kaidi amri watapigwa kijeshi.
Mkoa wa Ituri umeshuhudia machafuko ikiwemo mauaji ya watu kwenye vijiji pamoja na kushambulia baadhi ya kambi za wakimbizi wilayani Djugu.