DRC NYIRAGONGO

MTOTO MMOJA AUWAWA KINOGO WILAYANI NYIRAGONGO KIVU KASKAZINI.

news image

Sifa Shamavu nimtoto wa miaka mitatu na mkaazi wa kijiji Byungo kinogo wilayani Nyiragongo amepatikana nyumbani akiwa amefariki dunia baada ya kunyongwa na watu wasiyo julikana.

Mwili wake usio kuwa na uhai ulikutwa umetupwa barabarani meta miya moja na hamsini karibu na kanisa la watu wa sabato .

Taarifa toka sehemu za kinogo zasema kwamba, mtoto huyo musichana alipoteya kutoka nyumbani kwao tangu siku ya ijuma tarehe moja February elfu mbili ishiri na nne kwa saa za mchana Kati na kujielekeza mahali pasipo julikana. Fununu nyingine tulizo zipata sehemu hiyo, zaripoti ya kwamba kuna jamaa mmoja aliye muogota sehemu fulani akitangatanga njiani na kumu achiliya baadaye. Baada ya siku mbili yakukosekana kwake, mwili wake wakutwa umetupwa barabarani swala linalo wahuzunisha wakaazi na eneo Hilo.

Uchunguzi ume anjishwa kwa kwa ajili ya kufahamu kisa na kiini cha mauaji hayo ya mtoto muchanga. Jamaa aliye jidai kumutazama mahali fulani mtoto huyo ameshikiliwa na viombo vya usalama kwa ajili ya kufwatiliya uchunguzi. Mwili wa mtoto huyo, umepelekwa kwenye chumba cha kuhifazi maiti .

NDIWELUVULA BIN MUTUME MTV NEWS Online