TANZANIA

MTOTO AUZA NDIZI KUENDESHA FAMILIA YAKE INAYOMTEGEMEA

FEBRUARI 04, 2024
Border
news image

Chama Cha Mapinduzi CCM kimejitolea kumsomesha mpaka atakapomaliza masomo yake mtoto wa kiume aliyejitambulisha kwa jina la Alhaji Yahya Abdallah mkazi wa Masanga ambaye mama yake ni mgonjwa wa kuvimba tumbo na kumsaidia mama yake kulipiwa kodi ya nyumba kwa mwaka mzima huku akipatiwa matibabu pamoja na Bima ya Afya.

Kauli hiyo ya CCM imetolewa na Katibu wa NEC Itikadi , Uenezi na Mafunzo CCM Paul Makonda wakati akiongea na wananchi wa mkoa wa Kigoma ambapo mtoto huyo alijitokeza mbele ya umati wa watu nakuomba msaada wakusaidiwa kupata elimu ili anapokua baadae aweze kuisaidia familia yake ambayo kwasasa haijiwezi na yeye anakosa masomo.

" Tunafanya haya yote kwakua tuna mama mwenye upendo na watu wote bila kuwabagua na huyu si mwingine ni Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na ahadi zake anazowapa watanzania atawasaidia wengi bila ubaguzi kwakua wote wake" alisema Makonda.

Makonda alimkabidhi mtoto huyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mjini Ndugu. Salum Kalli kumsimamia.

Makonda amemchangia kijana huyo Kiasi cha Tsh Milioni 1,000,000/= kwa ajili ya kumuwezesha kijana huyo kupata sare, madaftari, vitabu , viatu na begi kwaajili ya masomo.

Pia, Mwenezi Makonda amewachangisha Viongozi na Watumishi wa Chama na Serikali kumsaidia Mtoto huyo na kuwezesha kupatikana kwa Kiasi cha Tsh Milioni 1,200,000/=.

Aidha, Amemuagiza Mkuu wa Wilaya wa Kigoma Mjini Ndugu. Salim kumtafutia shule ya karibu mtoto huyo na kuhakikisha Mama wa mtoto huyo anapatiwa Bima ya Afya yeye na mwanae.

MTV Tanzania