TANZANIA

MSAFARA WA MAKONDA WAPATA AJALI MTWARA

FEBRUARI 11, 2024
Border
news image

Msafara wa Katibu NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda umepata ajali leo 11.02.2024 Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.

Ajali hiyo imetokea majira ya Saa 9 Alasiri imehusisha zaidi ya magari 7 yaliyokuwepo katika msafara wa Ndugu Makonda uliokuwa unatoka mkoani Ruvuma kuelekea Jijini Dar es salaam.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza watu wasiopungua 2 wamejeruhiwa na kukimbizwa hospital ya mkoa wa Mtwara, na hakuna kifo chochote.

Kwa upande wa hali ya kiafya ya Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Paul Makonda ipo salama kabisa.

MTV Tanzania