DRC

DRC MONUSCO YAFUNGA KAMBI YAKE YA KAMANYOLA KIVU KUSINI MASHARIKI MWA CONGO DRC.

JANUARI 30, 2024
Border
news image

Katika sherehe zilizo shirikisha viongozi wa serikali na mkuu wa MONUSCO nchini DRC ,Umoja wa Matifa MONUSCO umefunga rasmi kambi zake katika Mji wa Kamanyola na Sange Kivu Kusini ikiwa ni mwanzo wa Bonde la Ruzizi.Akizungumuza wakati wa sherehe hizo zilizo huzuriwa na naibu gavana wa Kivu Kusini ,Mkuu wa MONUSCO nchini , Bintou Keita amesema kambi hiyo inayo patikana karibu na mpaka wa DRC na Rwanda inakabidhiwa kwa polisi ya congo PNC kulingana na maafikiano ilio afikiwa NEWYORK siku zilizo pita.

MONUSCO nchini DRC imeanza kuondoka na kufunga baadhi ya ofisi zake Kivu Kusini na Kivu Kaskazini kufatia makubaliano na serikali ya DRC .maafikiano inayo sema kuwa mwaka huu wa elfu mbili ishirini na nne Umoja wa Matifa hasa MONUSCO wote wataondoka DRC ili serikali yenyewe ichukuwe majukumu yake ya kulinda usalama wa raia wake .

MONUSCO imekuwa na wanajeshi wengi nchini DRC wanajeshi ambao walalamikiwa na raia kuwa wameshindwa kulinda na kukomesha mauaji dhidi ya raia mashariki mwa Congo ambako Vita vya pamba moto kati ya seriali na M23 .kuliko makundi ya waasi kupungua lakini uwepo wa MONUSCO uliongeza makundi ya waasi ,n ahata mauaji yakifanyika pambeni ya kambi zao kama vile wilayani Beni hasa Mavivi na mayimoya ambako wapiganaji kutoka kundi la ADF wamekuwa wakiuwawa wananchi kwa Zaidi ya miaka kumi na tano na kuwateka wengine hadi misituni katika uangalizi wa kikosi cha UN .

Tume ya umoja wa Mataifa nchini DRC ni miongoni mwa misheni ambazo zimetumia pesa nyingi sana bila mafanikio wakisema wakaazi wa Mikoa ya Ituri,kivu Kaskazini na Kivu Kusini.lakini kwa upande wa MONUSCO wakisema walifanikiwa katika utendaji kazi wao kuwalinda raia wa Congo dhidi ya mashambulizi.

Kuondoka kwa MONUSCO nchini DR. kuna pongezwa na serikali Pamoja na wananchi wa chini hasa wale wa vijijini ambao wapitia hali ngumu ya kimaisha na ambao kwa sasa wako katika kambi katika uangalizi wa Umoja wa Mataifa.

AM/MTVĀ DRCONLINE