Ni tangu alfajiri ya Jumapili Julai 14, 2024 milio ya risasi imesikika, inaashiria mkazi wa eneo hilo ambaye anasema hajui sababu halisi za milio hiyo. , akizungumza kuhusu mapigano hayo mkaazi asema hofu inasukuma wakaazi wengi kujifungia majumbani mwao japo wengi walikuwa wamejipanga kwenda kanisani.
Vyanzo vingine vinaripoti uwezekano wa mapigano kati ya waasi wa M23 na kundi lenye silaha ambalo ni vigumu kulitambua kwa sasa.
Kwa wiki kadhaa, Mji wa Kirumba umekuwa chini ya ushawishi wa uasi wa M23 unaoungwa mkono na Rwanda. Siku chache baadaye, Mareka iliomba usitishwaji wa mapigano kwa muda kwakupisha misaada kwa waathirika wa mapigano ambao wengi ni watoto na wanawake wanao ishi bila misaada katika miji mbali mbali ikiwemo Butembo .
Usitishwaji unao onekana kuvunjwa.