TANZANIA KIGOMA

MKUU WA MKOA WA KIGOMA AITA WATUMISHI WA AFYA KUTOA HUDUMA KWA WELEDI NA MAADILI

FEBRUARI 21, 2024
Border
news image

Watumishi wa afya mkoani kigoma nchini Tanzania wametakiwa kufanya kazi yakuhudumia wananchi kwa kuzingatia weledi wa taaluma yake ili kutoa huduma Bora za afya kwa wagonjwa, hii itatupa fursa Sisi yakuwafikisha wagonjwa hospitalini kwa mda unao faa, hospitali inaleta maendeleo na Ku wakusanya watu wa ngazi tofauti kama vile watumishi, wagonjwa...nk ,Alisema kiongozi wa mkoa huku akiwataka watumishi wa afya kufanya kazi kwa weledi na misingi iliyo wekwa na mukurugenzi, akiongeza kua ujenzi wa hospitali hii emepelekea serekali kua na deni ya ukarabati wa barabara inayo elekea ambapo hospitali hii ilipo.

Mkuu wa mkoa wa kigoma,kamishna jenerali mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokowaji Thobias Andengenye amesema hayo wakati akizindua jengo la jengo la wagonjwa wa nje nakuwaka jiwe la msingi katika hospitali ya manispaa ya kigoma ujiji ambayo imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.3 huku ujenzi wa majengo mengine ukiwa unaendele.

Kwa upande wa mganga mkuu manispaa ya kigoma ujiji,Hashim Mvogogo ameeleza gharama za mradi kua inakadiriwa kua bilioni 4.5,

Feza walizo zipokea kwa awamu ya kwanza na ya pili ni bilioni 1 na milioni 300;

Kwa ujumla zilipokelewa bilioni moja na milioni mia tatu ;na feza zilizo tumiwa ni milioni 546 ikibaki milioni 753 zinazo endelea kutumiwa kwa kuboresha ujenzi wa hospitali hiyo.

Baadhi ya wakaaji wa manispaa ya kigoma ujiji mkoani kigoma wanaonesha furaha yao kufuatana na ujenzi wa hospitali hii kwani hapo awali walilazimika kutembea umbali kutafuta huduma za afya pamoja na wajawazito kujifungulia njiani : mwanzo tulikua n'a shida ya usafiri, wanamama walikua napata tabu waki kifungua njiani wakienda hospitalini,lakini baada ya raïs mama SAMIYA kuingia ametukumbuka, changamoto iliokuwepo ,ilikua kufata huduma za afya mbali;walisema wananchi Hao.

Kwa mda mrefu wananchi katika manispaa ya kigoma ujiji wamekua wakitumia vituo vya afya pamoja na hospitali ya rufaa ya mkoa wa kigoma maweni kwa ajli yakupata huduma ambapo hâta hivyo kwa mjibu wa baadhi ya wananchi, baadhi ya ndugu Zao walipoteza maisha kutokana na huduma za afya kua mbali na makazi yao.

MTV Tanzania