DRC

Mkuu wa Majeshi ya JWTZ Atembelea Mustari wa Mbele wa Mapigano Mashariki Mwa Congo

MACHI 02, 2024
Border
news image

Akiwa katika kikao cha makamanda wa Mataifa ya kusini mwa Africa SADEC Generali MKUNDA mkuu wa majeshi ya Tanzania akiwa na ukakamavu ametembelea uwanja wa mapigano katika Mji wa Sake kivu kaskazini ambako wanajeshi wa Tanzania walijeruhiwa baada ya kutupiwa bomu na waasi wa M23 kutoka kwenye milima ya SAKE .MKUNDA alikagua kambi ya kijeshi ya Mumbambiro ambako amekuwa na kikosi chake kinacho shirikiana na na wanajeshi wa Congo FARDC katika mapigano dhidi ya waasi wa M23.

JWTZ ama jeshi la Tanzania lip DRC katika kikosi cha SADEC ambao lengo kubwa nikuwapa amani na usalama wananchi wa Congo hasa kuulinda Mji wa GOMA.Wanajeshi wa Tanzania wamekuwa wakitishiwa na M23 kuwa itawakamata ama kushambulia na vifaa vyao japo kuna wanajeshi wengine katika SADEC hasa Africa Kusini na Malawi ambao wote wanaandamana katika juhudi za kuhudumisha amani kwa nguvu Kivu Kaskazini.

Mji wa Sake upo Kilometa Ishirini magharibi mwa mji wa Goma pambeni na ziwa Kivu eneo lake la kusini na mbunga la Virunga eneo lake la kaskazini Pamoja na milima ya Masisi ,milima inayo dhibitiwa na M23 na washirika wao ambao serikali ya DRC inasema Ni Rwanda .hivi karibuni Umoja wa Matifa MONUSCO ulishutumu Rwanda kuwapa wanajeshi wa RDF NA silaha nzito waasi wa M23 AMBAO washutumiwa kwa amauaji na kukiuka haki za binaadamu hasa kupelekea maelefu ya wakaazi kuhama vijiji vyao .Wilayani Masisi,Rutshuru na nyiragongo.

M23 ikisema mapigano mashariki mwa Congo itasitishwa iwapo serikali ya Kinshasa itakubali mazungumuzo ya moja kwa moja,swala ambalo serikali imekuwa ikitupilia mbali kwamba haiwezi kufanya mazungumuzo kwan I DRC imepitia mazungumuzo tangu AFDL ,CNDP,M23 hata wakati wa RDC.

Wakaazi wakiomba Rais serikali yake kuganya juhudi zote kuhudumisha amani ili wakimbizi wote warudi nyumbani kwao kuendelea na kilimo.

AM/MTV DRC ONLINE