TANZANIA
Mkutano Kati ya Spika wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson na Ujumbe wa Kamati Ya Kilimo, Maji, Maliasili na Mazingira wa Iran
SEPTEMBA 5, 2023
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Kamati ya Kilimo, Maji, Maliasili na Mazingira kutoka Bunge la Jamhuri ya Kiislam ya Iran Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 5 Septamba, 2023.
Ujumbe huo umeongozwa Mhe. Rahmatollah Norouzi, Mbunge wa Bunge hilo akiwa ameambatana na Mhe. Hossein Alvand, Balozi wa iran nchini Tanzania.