TANZANIA

MKOA WA DODOMA WABAINISHA VIPAUMBELE VYAKE 2024

JANUARI 22, 2024
Border
news image

Mkoa wa Dodoma nchini Tqnzania umeweka wazi vipaombele vyake kwa mwaka 2024 ikiwa ni pamoja kuimarisha sekta ya kilimo inayochangia asilimia 40 ya pato la Mkoa huku sekta nyingine zikiwa Utalii, viwanda, madini, usafirishaji kama shughuli za kiuchumi pamoja na kuimarisha elimu na mazingira. Pamoj na utoaji huduma kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati akifungua kikao na viongozi wa dini wa Mkoa wa Dodoma wenye lengo la kushirikiana katika kufikia vipaumbele hivyo.

"Rais wetu amefanya kazi kubwa na ya kipekee kwa kuwa anajali watu wa chini. Serikali imetoa kiasi cha jumla ya Shilingi Bilioni 95 kwa ajili ya kutekelezwa miradi ya Kilimo Wilaya ya Chamwino, Mpwapwa na Bahi. Miradi hii Ina lengo la kuimarisha kilimo cha kisasa cha umwagiliaji kwa mwaka mzima.

"Tunahitaji Dodoma iwe kitovu cha usafirishaji ili kuinua Uchumi kwa haraka na kuwa Mji wa kimkakati. Kwenye Utalii, tuna vivutio vingi na tunahitaji Sasa wawekezaji wakubwa kwa ajili ya kujenga Hoteli zenye hadhi ya nyota 5 ambazo zitawezesha kupokea wageni kutoka mataifa mbalimbali" Ameeleza Mhe. Senyamule

Akiwasilisha taarifa ya Elimu kwa Mkoa wa Dodoma, Afisa Taaluma Mwl. Justin Machela amesema Mkoa umejiwekea Mkakati wa Elimu 2024.

"Mkakati wa Elimu Mkoa umejikita katika kuinua ubora wa elimu na ufaulu shuleni ikiwemo kutokomeza utoro. Kwenye matokeo ya mitihani ya Taifa tumedhamiria; Elimu ya msingi ufaulu ufikie 95%,, kidato cha 4 ufikie 65%, kwa kupata madaraja ya I -111 huku kidato cha 6 yafikie 100% kwa ufaulu wa madaraja 1-11 tu.

Kikao cha Mkuu wa Mkoa na viongozi wa madhehebu ya dini wa Mkoa kina lengo la kushirikiana katika kufikia vipaumbele vya Mkoa kwani viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya ushawishi kwa waumini wao ambao ndio wananchi wa Dodoma kwakua viongozi wa Serikali wanafanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na viongozi wa dini.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania