DRC/GOMA

SHUGHULI MBALI MBALI ZIMEKWAMA MJINI GOMA KUTOKANA NA MGOMO WAENDESHAJI PIKIPIKI

JANUARI 29, 2024
Border
news image

Ni tangu asubui ya kuamkia leo juma tatu ishirini na tisa elfu mbili ishirini na nne ,magari, pikipiki na uchukuzi binafsi ukisimama katika Mji wote wa Goma kufatia mwito ulio tolewa na kamati za waendeshaji pikipiki wakipinga hatua ya mea wa GOMA,alie piga marufuku utumiaji wa taxi za pikipiki kuanzia saakumi na moja za jioni kutokana na usalama.

Hatua hii imeonekana kuungwa mkono na raia wakiomba serikali kuchukuwa hatua ya ulinzi kuliko kuzuia watu kusafiri na pikipiki jioni ikiwa ndio usafariki wa haraka na nafuu kwa wakaazi wa Goma.

Utafahamu kwamba hatua hiyo ilichukuliwa na mea wa GOMA kufatia ukosefu wa usalama kila jioni majambazi wanao kuwa na silaha wakitumia pikipiki baada ya wizi ama mauaji ya watu na vile kupunguza vitisho kutoka waasi wa M23 ambao kwasasa wana zunguuka Mji wa Goma.

Madereva walitangaza wiki iliyopita, mgomo huo, kulingana na wao, una nia ya kwenda vitani dhidi ya hatua ya meya, ambayo wanaelezea kuwa haifai kwa maisha yao ya kiuchumi na familia.

wakaazi wakishutumu baadhi ya wana usalama kukiuka sheria na kuwanyanyasa wananchi , nyakati za jioni.

Hali hii imejiri wakati Meya wa Mji alikuwa amepiga marufuku mgomo huu.

Nadège Kahindo -MTV GOMA DRC