DRC GOMA

Meya wa Mji wa Goma Kivu Kaskazini atangaza kuwakamata majambazi wenye silaha wanao waua watu kwa saa mchana Mjini Goma.

Aprili 11, 2024
Border
news image

Akizungumuza na wanahabari kwenye ofisi kuu ya Mji wa Goma meya wa Mji asema watu wenye silaha walio husika na mauaji ya watu hii juma tano wamekamatwa ,miongoni mwao wanajeshi Tatu wa serikali ,wazalendo wa wili Pamoja na raia walio kuwa wakishirikiana nao katika ujambanzi.

Hii imejiri baada ya malalamiko makali ya wakaazi wa Goma kulalamikia usalama ambao kwa sasa ni tatizo kubwa ,Goma ikishuhudia mauaji na milio ya risasi kila siku Mjini kwa saa za Jioni ama usiku .mauaji inayo tekelezwa na watu wenye silaha wanao valia uniform ya kijeshi na zile za wazalendo.

Wakaazi wameomba serikali kuchukuwa hatua mazubuti na kupeleka wanajeshi wote kwenye uwanja wa mapigano kuliko kuhangaika Mjini ambako hhuanza kunyanyasa wakaazi na kuwatisha kwa silaha. Katika Mji wa Goma Maisha imekuwa tataizo kubwa kila mmoja akiishi katika uhoga na silaha zikiwa nyingi. Wananchi wakiomba sheria mpya za kuwanyonga wahalifu kuanzia wanajeshi hao wa serikali walio kamatwa na Vyombo vya usalama ambao wamejigeuza kuwa mabandia.

Uongozi wa Mji umesema walio kamatwa watafikishwa mahakamani na kusambishwa hadharani mbele ya wakaazi kufahamu nani alie watuma kuwaua wafanya bishara Mjini Goma.

AM/MTV DRC ONLINE .