DRC/KIVU KUSINI

Mashirika ya kiraia Katika Mji wa Bukavu mkoani Kivu Kusini waomba wananchi kushiriki Mgomo wa siku tatu kupinga unyanyashwaji kutoka vyombo vya polisi wa barabarani.

Aprili 08, 2024
Border
news image

Katika Mkutano ulio fanyika hii juma pili katika mji wa bukavu masharika ya kiraia imesema polisi wanao husika na uslaama barabarani imekuwa ikinyanyasa madereva na watu wa taxi nah ii kuathiri sana shughuli za usafiri katika Mji wa Bukavu .Polisi kwa upande ikisema iinafanya hivyo kuweka utaratibu katika usafiri mkoa wa Kivu Kusini hasa kuweka kila mumiliki wa gara awe na vitambulisho..

Habamungu Mratibu wa shirika za kiraia Kivu Kusini asema iwapo polisi haita rekebisha hatu ahii wkaaazi katika Mji wa Bukavu wataanzisha mgomo wakufunga shughuli za taxi hadi suluhu litakapo patikana na polisi kupana maelezo Zaidi kwa raia wa Mji wa Bukavu kuhusu hali ya unyanyashwaji wa watumiaji wa magari ya moto na pikipki ambazo ndizo za saidia usafiri wa uma katika Mji wa Bukavu Kivu kusini.

Shirika za kiraia zasema zimepokea malalamiko mengi ofisini mwake kutoka madereva na watumiaji wa Taxi Katika Mji wa Bukavu ndio sababu wameamua kuanzisha Mgomo wa siku tatu hadi kuwe na maelewano kati ya vyomvo vya usalama barabarani na wakaazi . Habamungu anasema usumbufu wa polisi wa barabrani unasabisha watu kuchelewa kwenda shuleni na hata kazini .

Wanao alikwa kushiriki mgomo wakiwa hasa watu wa Taxi Mjini Bukavu. Serikali kwa upande wake ikiomba wakaazi kuendelea na kazi zao kama kawaida kwani ni majukumu ya serikali kuhakikisha kila anae tumia gari.pikipiki ama vifaa vingine vya moto kuwa na vibali .

Nadège Mulemba.