DRC - BUTEMBO

Masharika ya kiraia na makundi ya vijana katika Mji wa Buntembo yaandamana na kutembea kilometa Zaidi ya thelathini hadi Mji wa Musienene wilayani Lubero kupinga uasi wa M23

JULAI 15, 2024
Border
news image

Akizungumuza na MTV katika mji wa Butembo ROSE KAHAMBU tuombeane amasema lengo kubwa la maandamano yao nikuonesha waasi wa M23 na Umoja wa Matifa kwamba hawataki kuongozwa na uasi wa M23 ,Rose ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa umekaa kimia kuhusu matatizo wanayo pitia wananchi wa Congo kutokana na uasi wa M23 .

Rose Kahambu tuombeane akiwa mwanaharakati wakutetea haki za binaadamu na wanawake Katika Mji wa Butembo Kivu Kaskazini amekuwa miongoni mwa wakaazi wa Mji wa Butembo ambao wametembea kilometa Zaidi ya ishirini kutoka Butembo hadi Mji wa Muisenene wilayani Lubero kupinga uasi wa M23 Mashariki mwa Congo na kuomba UN kuwajiba na taifa Jirani la Rwanda kuondoa wapiganaji wake kwa haraka .

Maandamano hayo yanajiri wakati ambapo kuna baki siku nne kabla ya kumalizika kwa muta wa usitishwaji wa mapigano ulio ombwa na serikali ya Marekani ,wakaazi wa Mji wa Butembo na Lubero wakiomba amani na usalama na kuunga mkono juhudi za jeshi la serikali kupambana na uasi wa M23 ambao serikali ya Kinshasa inasema wanaungwa Mkono na Rwanda ,Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya hivi karibu ilionesha kwamba Rwanda na Uganda inaunga mkono juhudi za waasi wa M23 kuteka miji na vijiji mashariki mwa Congo DRC.

Wengi wao wakiwa ni vijana na wasichana washutumu umoja wa Mataifa Pamoja na taasi nyingine za kimataifa n ahata MONUSCO kukaa kimia kuhusu mateso wanayo pitia wakaazi wa Kivu Kaskazini ,Vijana wakibeba mabango wametembea safari ndefu kwa Migu kama halama ya kuonesha hathira zao kuhusu vita wanavyo viita vya uvaamizi.

Marekani ikiomba pende zote kusimamisha mapigano na kuelekea kwenye njia ya mazungumuzo.

AM/MTV News DRC