DRC

Mapigano Makali Yameripotiwa Kati ya Wapiganaji Wazalendo na Waasi wa M23 Kwenye Milima ya Shasha Wilayani Masisi Serikali ya DRC Ikisema Wanaungwa Mkono na Rwanda

FEBRUARI 25, 2024
Border
news image

Wakaazi katika Mji wa Minova wasema tangu saakumi na moja silaha nzito zilisikika kwenye milima ta Ngumba karibu na Mji wa Shasha unao dhibitiwa na waasi wa M23 hii juma pili .wakaazi walio kuwa karibu na vijiji hivyo wakimenya mbio kuhufia Maisha kutokana na bomu zenye kuangua hap ana pale.

Wapiganaji wazalendo wakiungana na jeshi tiifu kwa serikali FARD wakijaribu kuzuia waasi walio kuwa na lengo la kuendelea kuteka vijiji vingine wakati jumhia ya kimataifa imekuwa ikiomba pande zote zinazo twangana kusimamisha mapigano hayo ambayo imepelekea Malefu ya watu kuhama makaazi yao na kuwa wakimbizi katika taifa lao.Hadi sasa matukio ya mapigano hayo haijajulikana kutokana kwamba eneo hilo wakaazi wengi wamesha ham ana kukimbia makaazi yao hadi Mji Jirani wa Minova unao patikana kaskazni mwa eneo la mapigano.

Mwanzoni mwa wiki Rais wa Congo Felix Tshisekedi alisema yuko tayari kushiriki hatua zote za mazungumuzo ,bila kuzungumuza na M23 ambao amesema ni Rwanda inayo waua raia wa Congo kupitia M23 .M23 imekuwa ikisema kwamba wanacho kihiyaji ni mazungumuzo ya moja kwa moja na serikali ya Kinshasa lakini serikali ya Kinshasa ikisema inaweza kuzungumuza na Rwanda bila M23 .

Wiki hii Rais wa DRC anasubiriwa Angola kukutana na msuluhishi wa Mzozo wa Congo kuchukuwa maelekezo mapya kuhusu mikataba mbali mbali ilio wekwa kwa ajili ya amani na usalama mashariki mwa DRC na Kanda ya maziwa makuu.wachambuzi wakiwa na hoga ya kuzuka vita vikubwa maziwa makuu iwapo mzozo huu hauta tatuliwa kwa haraka.

AM/MTV DRC ONLINE